Sherehe za kumuapisha
Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (pichani), Waziri
Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitafanyika katika Ikulu ndogo
ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2015 kuanzia saa 4.00 Asubuhi.
Sherehe hizo
zinafanyika siku moja baada ya Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha jina lake kwa kura nyingi kuwa Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia uteuzi uliofanywa na Mhe. John
Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba
ya sherehe hizo, Wageni waalikwa wote wanapaswa kuwasili katika Ikulu ya
Chamwino kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.
Sherehe hizo
zinatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu wastaafu na
waheshimiwa wabunge.
Imetolewa
na Idara ya Habari MAELEZO
19
Novemba, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...