Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili mjini Dodoma kwa ajili ya kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu itakayojadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa ujumbe katika Twitter ya Chama cha Mapinduzi Kamati kuu imewapitisha Ndg Job Ndugai, Ndg Abdallah Mwinyi na Dkt Tulia Ackson Mwansasu kugombea nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wana CCM alipowasili mjini Dodoma kwa ajili ya kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu itakayojadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Job ndugai anafaa kua spika sababu anaviweza vishindo vya wabunge
ReplyDeletesana sana, apite bila kupingwa
ReplyDelete