Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kushoto) akijadiliana jambo na Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise (katikati). Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile.
Wajumbe wa kikao wakimsikiliza katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi (kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia). Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi.

Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zimeagizwa kutochelewesha kushughulikia maombi ya wawekezaji pale wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wanapoonesha dhamira ya kuwekeza. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati wa kikao chake na Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo.

Mhandisi Chambo aliwaagiza watendaji hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea, na badala yake wazingatie Sheria na maadili ya kazi zao, kutokana na ukweli kwamba sekta ya Nishati ni sekta nyeti inayohitaji watendaji waadilifu na wabunifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. TUnataka kujua walivotoka hapo waligawana posho ya vikao? hiyo njoo kesho mbona bado ipo hapo Tanesco labda iishe jana !

    ReplyDelete
  2. Maoni yangu yanaenda kwa EWURA ambao nafikiri ndio mdhibiti wa nauli za mabasi yaendayo mikoani kama sijakosea.

    Kipindi cha mwisho wa mwaka huwa mabasi mengi hupandisha nauli kwa abiria sababu ya uhitaji wa wengi kusafiri, hii ni kero sana kwani hata mimi ilishanikumba na imenichukiza sana baada ya kujua kumbe sio halali.

    Maoni yangu ni kwamba nauli halali ambazo zimetangazwa na mamlaka husika zibandikwe kwenye mabasi yote yaendayo mikoani ili abiria anapoingia kwenye basi ajue analipa kiasi gani isiwe tu ni mazoea. Pia nauli hizo zibandikwe kwenye mbao za matangazo za stendi kuu ili abilia wasirubuniwe na wapiga debe au baadhi ya makondakta wasio safi.

    Naitwa Bw. Finehas Ruhiye

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...