KWAYA ya Wakorintho wa Pili ya Wilayani Mafinga mkoani Njombe, imekuwa
ya kwanza kuthibitisha kushiriki Tamasha
la Kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema
uongozi wa kwaya hiyo umekubali kushiriki katika tamasha hilo baada ya uchaguzi
Mkuu uliofanyika Oktoba 25 nchini kote.
“Kwaya ya Wakorintho wa pili wameanza kuthibitisha kushiriki tamasha la
Shukrani baada ya kufanyika uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, tunaendelea na
maandalizi ya kufanikisha tamasha hilo ambalo litashirikisha idadi kubwa ya
Watanzania,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema katika
tamasha hilo, Kwaya hiyo itafanya uzinduzi wa albamu yake ya Mchepuko sio dili yenye
nyimbo nane.Nyimbo zilizoko kwenye albamu
ya Mchepuko sio dili ni pamoja na Tanzania, Mchepuko sio dili, Watenda mabaya,
Eee bwana, Tuokoe baba, Dunia hii, Yahwe Tunakuinua na Hana.
“Kwaya ya Wakorintho itafanya matukio mawili katika
tamasha hilo, la kwanza ni kushiriki Tamasha la Kushukuru na la pili ni
kuzindua albamu yenye nyimbo nane,” alisema Msama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...