Habari kaka Michuzi,
Naomba unifikishie katika blog yako maana naamini mpaka vyombo husika vitaliona hili.

Tarehe 16/11/2015 nilikua napita njia ya Kilwa,nilipofika mivinjeni nikakutana na hilo Gari la kubeba contena kama linavyoonekana katika picha,nikiwa nyuma yake likaingia Barabara ya vumbi iendayo bandarini kupitia Yara, nilimpigia sana honi na kumuwashia Taa huyo dereva asimame afanye taratibu za maksudi kunusuru uhai Wa RAIA wengine ila alikaidi,alishuka utingo wake akaangalia na kuendelea na safari, kiukweli lile kontena lilikua nje ya lock zake na lilikua likicheza sana kwenye njia ya vumbi na cha kushangaza kabisa lilipofika barabara ya bandari/shimo la udongo kulikua na traffic wanne barabarani lakini hawakuchukua hatua yoyote ile zaidi ya kuliangalia tu.

Tutaendelea kupoteza ndugu jamaa n marafiki zetu mpaka lini kwa uzembe Wa watu wachache wasiojali uhai wa wengine?

Wako Mdau.
 Lori hilo likikata kona kutokea barabara kubwa kuelekea bandarini kupitia Yara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii hatari sana! uzuri Kamanda Mpinga huwa anazungukia kwenye mitandao I hope atakua kaiona hii na kuchukua hatua muafaka!

    ReplyDelete
  2. The mdudu, watu wazembe kama wewe mdau uliowaona siku nyingine wapigie mayowe kwa raia wema lazima wangesogea ulipo kisha unawaambia hawa watu wameingia huku na mgari wao mkubwa unaocheza ili udondokee watu au magari mengine lazima raia wema pamoja na wewe mngetoa kipigo cha mbwa ili iwe fundisho kwa washenzi kama hao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...