Neno Dudumizi si geni katika masikio ya watu wengi. Hapa kwetu Tanzania, Dudumizi inamaanisha ni ndege, ndege huyu mwenye rangi ya ugoro na nyeusi akiwa na macho mekundu ni adimu sana hasa kwa watu wanaoishi mijini, hii inaweza kutokana na uchache wake au mazoea ya ndege huyu. Pia, kwa upande wa pili, neno Dudumizi ni kampuni bora inayojishughulisha na masuala ya huduma za IT kama kutengeneza websitekutengeneza systems za kompyuta na application za simu.

Watu wengi wanaposikia jina Dudumizi kama kampuni, kitu cha kwanza ni mshituko unaoambatana na swali moja, Kwanini tumeamua kuiita kampuni yetu Dudumizi? Kwa wengi, neno Dudumizi bado si neno rafiki huku likihusishwa na mambo mengi sana ambayo si mazuri, na mengi ni imani na si uhalisia, ila kwa upande wa mazuri, Dudumizi ana mengi sana ya kuyachukua kwenye IT.

Hebu tuangalie sifa za ndege huyu anayeitwa Dudumizi. Ndege jamii ya Dudumizi ana sifa kubwa tatu.
1. Dudumizi huwa na mlio tofauti unaoashiria kuwepo kwa uwezekano wa kunyesha mvua.

2. Kiota cha Dudumizi hakijafungwa, na mara nyingi huwa kwenye pachipachi ya mti, hii humrahisishia Dudumizi kukipanua kadri awezavyo bila kuvunja au kuhama, tofauti sana na ndege wengine ambao viota vyao vimefungwa na kutotoa mwanya wa upanuaji.
3. Kiota cha Dudumizi kimejazwajazwa majani na mara nyingi unaweza kudhani ni mrundikano wa majani na siyo kiota, pia kwakuwa kipo wazi, Dudumizi huweza kumuona mvamizi au adui tangu akiwa mbali,hivyo humsaidia kujikinga na wavamizi.

Hizo ndizo sifa kuu za ndege Dudumizi, je sifa hizi zina uhusiano gani na IT. 

1. Ubunifu na uvumbuzi (Innovation): Kwenye IT kuna kitu tunaita Ubunifu wa utendaji au uvumbuzi (Innovation), uvumbuzi huja baada na kufikiria halafu kutenda, kwenye kitabu chake cha Anza na kwanini (Start with Why), mwandishi Simon Sinek amesema, huduma au bidhaa haiwezi kuwa na ubunifu kama huduma hiyo haijaweza kubadili mfumo wa ufanyaji kazi. Mfano mzuri, ni jinsi gani kampuni ya Apple ilivyoweza kubadili matumizi ya simu kutoka button nyingi hadi moja. Na ubinifu husukumwa na mahitaji ya sasa au ya kesho.
 Kama Dudumizi anavyoweza kubashiri ujio wa mvua na kujiandaa, na sisi kwenye IT tunatakiwa kuwekeza kwenye ubinifu na kuja na huduma zinazokidhi mahitaji ya Mtanzania kwa wakati wote (leo na kesho). Na hii ndiyo sababuDudumizi tumeanza kuja na bidhaa zenye kulenga kubadili mtindo wa ufanyaji kazi, Michongo ni moja ya bidhaa yetu ya kwanza kwenye mlengo huu.
 

2. Ukuaji (Scalability): Dunia ya leo si dunia iliyo simama wala kujitosheleza. IT ikiwa muongozaji mkuu wa ufanyaji kazi, ni lazima iwe na uwezo wa kukua na kupanuka kulingana na uhitaji(scalability). Chukulia mfano leo hii umeamua kutengeneza System inayokuwezesha kurekodi maudhurio ya wafanyakazi, kwa sasa una wafanyakazi mia moja tuu, je hali inakuwaje endapo kampuni imekua na sasa inahitaji kuwa na huduma nyingi zaidi na sasa kuna wafanyakazi laki moja?? Je unatakiwa kuanza upya au kuendeleza ulicho nacho??
Tumekuwa tukiona watu wengi wakuchajiwa pesa zaidi na zaidi sawa na kuanza upya pindi wanapotaka kuongeza kitu fulani kwenye website au system. Na mara nyingi hii hutokea pindi unapotaka kuongeza uwezo wa system (feature), mkataba unasemaje kuhusu ukuaji?? Je ulijiandaa kwa hili?
 Dudumizi hujiandaa kwa kuwa na kiota kilicho tayari kupanuka, na kwa mtindo wa ujengaji wa Dudumizi, hata kama ataamua kuhama basi hasumbuki kuanza upya kutafuta zana, tayari anazo na zinamuwezesha kukua atakavyo. 
3. Usalama (Security): Katika maisha ya binadamu, usalama ni kitu cha lazima, na usalama huu siyo tu wa maisha pekee, bali na kila kitu kinachomzunguka au anavyovihodhi binadamu huyu. IT ni moja ya vitu muhimu kwa binadamu wa dunia ya leo. Usalama wa kiota cha Dudumizi unafanana na umuhimu wa usalama kwenye fani ya IT. Iwe ni kwenye Website, kwenye System au hata kwenye vifaa vya kieletronics. Kote tunakutana na kaulimbiu,"Usalama kwanza".
 

Kutokana na sababu hizo, sisi tukiwa kampuni ya IT, tena ya Kitanzania, ndiyo maana tumeamua kijiita Dudumizi. Na ufanyaji wetu wa kazi unaendana na mfumo kamili ya maisha ya Dudumizi. Hivyo, unapofanya kazi na Dudumizi, unakuwa na uhakika wa Ubunifu, Ukuaji na Usalama kama kauli mbiu yetu inavyosema, Fikiri. Gundua(Think.Innovate).
Katika makala zijazo tutaelezea maana ya Logo ya Dudumizi na ni jinsi gani ilivyoweza kuingiza Ubunifu wa Kitanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...