Na mdau Ruger Kahwa

Awali ya yote napenda kumpongeza Mh. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu alipokuwa waziri wa ujenzi alikuwa anonyesha dhahiri kuwa ana nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania, na sio maslahi yake mwenyewe na familia yake. 
Chama chetu cha CCM kilitambua hilo na kumpendekeza kuwa mgombea urais wa Tanzania. Naamini ndani ya chama kuna watu walikuwa na kiu na shauku ya kuwa marais kwa ajili yao na marafiki zao, lakini Mungu wetu hakuruhusu hili litokee. 
Hakurusu hilo litokee kwa sababu Mungu anayajua matatizo ya watanzania na ametupa mtu sahihi ili atukumboe. Katika kipindi kifupi tangu alipoapishwa kuwa Rais ameonyesha kasi ya ajabu na nia ya dhati ya kutaka kuwasaidia watanzania. 
Ziara zake za kushtukiza na jana kuamuru mamilioni ambayo yangetumika kwa party ya wabunge yapelekwe Muhimbili kununua vitanda ni ushahidi tosha wa nia yake ya dhati ya kuwasaidia Watanzania. 
 Mheshimiwa Rais, umeanza vizuri sana, na naomba uwabane watendaji wa ngazi zote kuanzia mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu wakuu,wakurugenzi,makatibu tarafa na kata na hata watendaji wa vijiji wafanye kazi , kwani wengi wao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kufanya siasa tu. 
Wananchi katika ngazi za wilaya, kata na vijiji wana shida nyingi. Na asilimia zaidi ya tisini ya shida hizo zinasababishwa au zinachochewa na watendaji wabovu au wazembe wanaofanya kazi kwa mazoea na manufaa yao binafsi. Nimeona wananchi wanadhulumiwa mali zao vijijini(hasa yatima na wajane), wanabambikiwa kesi. 
Watu wenye pesa wamekuwa wakinunua haki. Kwa kweli inaumiza sana. Mabaraza ya usuluhishi ya kata ndio kabisa, haki haipatikani ni posho kwa kwenda mbele. Kwa mtindo huu mtu maskini hapati haki. Hali ni ngumu. 
Wananchi tuna imani kubwa sana na wewe na kama ulivyosema hutatuangusha na sisi tunasema watendaji wako wasikuangushe. Kwa mantiki hiyo basi , itakuwa vyema ukapangua na kupanga safu yako vizuri hasa ngazi ya chini ya wakuu wa wilaya. Tukipata watu wa zuri na waaminifu katika ngazi hizo tutaanza na mwanzo mzuri . Katika ngazi hiyo tunataka watu wachapa kazi na sio wapiga siasa mchana kutwa. 
 Mungu ameipenda Tanzania na kutupatia kiongozi kama wewe, mcha Mungu,mchapakazi, mkweli na hanayechukia unafiki. 
Na sasa Mh. Rais tunaomba utupangie safu ya watu wacha Mungu, wachapa kazi, wakweli na wanaochukia unafiki, kwani msema kweli ni mpenzi wa Mungu. 
 Hata ikibidi ubadilishe asilimia tisini ya wakuu wa wilaya na viongozi wengine ni sawa tu, ili mradi watanzania wafaidike na matunda ya nchi yao wenyewe. Wewe ni zawadi kutoka kwa Mungu. Na wapenda haki wote tuko nyuma yako. 
 Asante

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ni mapema mno kusema lolote, kuongoza nchi si jukumu la mtu mmoja na hapa ndipo palipo na ugumu,tuombe atakao wachagua kumsaidia wawe na nia na mtazamo unaofanana.

    ReplyDelete
  2. Mola awalinde viongozi wetu wote wa awamu ya tano na awajaaliye uadilifu, uaminifu, ukweli na wawe committed katika suala zima la utendaji wao ili tufike pale tunapostahili na kuwa na Taifa zuri lenye tija kwa kila raia wake aliye ndani na nje ya nchi. Mungu ibariki Tanzania, viongozi na raia wake wote.

    ReplyDelete
  3. Absolutely true and intellectually written.
    Well done writter.

    ReplyDelete
  4. Rais ameonyesha mfano kiongizi anachitakiwa kufanya hivyo watakaochaguliwa wafanye kama yeye. Yeye hawezi kutembrlea kila mahali ni jukumu la hao wa chinibyake sas waoneshe makeke sio kukaa ifisini tu. Haipendezi rais i akafanya kila kitu eakati watendaji wapo.

    ReplyDelete
  5. Yule mwingine alikuwa chaguo la mungu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...