Na Kaka Mwinyi
Kundi mahiri kabisa la muziki wa mahotelini, Mambo Afrika
lenye maskani yake huko Dubai, Falme za Kiarabu, limezidi kujipngezea umaarufu
baada ya kutajwa katika orodha ya ‘Waburudishaji Bora’ wa mwaka.
Kundi hilo linaloundwa na wasanii kadhaa toka Tanzania na
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, limeingizwa katika orodha ya wadau wa masuala
ya burudani nchini humo kutokana na uwezo wake wa kuburudisha katika maonesho
mbalimbali linapoalikwa.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Giovanni King (pichani kulia), amesema
kuwa, Mambo Afrika inajivunia hatua hiyo aliyoilezea kuwaimarisha zaidi kwa
kufanya kazi nzuri na bora kila kukicha katika kukabiliana na ushindani mkubwa
uliopo kwa bendi na vikundi vya sanaa vinavyotumbuiza sehemu mbalimbali huko
Dubai.
“Kundi letu lina wasanii wachache sana. Tunaye muimbaji wa
kike Winfrida Masi ‘Winnie’, mpiga gitaa la besi Philip Kazamir na Miraji
Chocholi anayecharaza drums. Wengine ni wapapasa vinanda Angelus Lyampawe na
Johannes Lista na mimi mwenyewe (Giovanni). Tuko vizuri sanjari na wanenguaji
(dancers) ambao huwa tunawabadilisha mara kwa mara kulingana na mahitaji ya
nyakati,” akasema Giovanni.
Aidha, Giovanni aliyewahi kutamba na bendi ya Chuchu Sound
miaka ya mwanzoni ya 2000, amesema Mambo Afrika hufanya maonesho yake kwenye
klabu ya kimataifa ya Africana iliyopo ndani ya hoteli ya Palm Beach ambayo iko
kitongoji cha Bur-Dubai. Katika maonesho
yake, Mambo Afrika hupiga muziki wa aina zote.
Kundi mahiri kabisa la muziki wa mahotelini, Mambo Afrika lenye maskani yake huko Dubai, Falme za Kiarabu
Men in african, girls in western.
ReplyDelete