Na
Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la Wasanii nchini wamewataka mashabiki wao kuondoa tofauti za kiitikadi ambazo zilijitokeza katika kampeni waendelee kuwaunga mkono.
Akizungumza na waandishi wa habari,mmoja wa
msanii, Stara Thomas amesema kila watu walikuwa na itikadi katika kampeni hivyo
ni wakati mwafaka wa kufanya kazi.
Stara amesema wameshiriki katika kampeni
zimeisha sasa ni wakati kushiriki katika majukumu kama wasanii.
Hata hivyo amesema wanapongeza Rais wa Awamu ya
Tano, Dk. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa na watanzania katika kuongoza.
Nae Msanii Mkongwe, John Kitime amemtaka Rais
kuwekea umuhimu wa idara ya utamaduni
kuweza kufanya wizara kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi kwa
wasanii.
Kitime amesema idara hiyo kuhama hama
kumewafanya wasanii kuwa nyuma na kufanya nchi kushindwa kupata mapato licha ya
wasanii kuwa wengi.
Kwa upande Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga
Pepeta, Asha Baraka ameshauri Rais mpya katika uteuzi wa bodi wasanii wateuliwe
kutokana na uwezo wao katika kazi hiyo.
Asha amesema kuteuliwa kwa wasanii katika bodi
zenye sanaa nchini zitaleta chachu na wasanii watatambuliwa na jamii kwa
mchango wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...