Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini Dr.Suma Kaare amemtaka Raisi John Pombe Magufuli adhibiti upotevu wa mali asili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.
Suma Kaare amesema hayo katika mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili unaoendelea jijini Arusha,Kaare amesema kuwa jukwaa hilo litashirikiana na Rais huyo katika kuhakikisha kuwa maliasili zinalindwa na kuwanufaisha Watanzania kwa kiwango stahiki.
“Tunajua Rais wetu mpya ana kazi kubwa ya kulinda maliasili za nchi hii kama ilivyo kauli mbiu yake ya “kazi tu” tunaamini atazuia upotevu mkubwa wa rasilimali unaofanywa na watendaji wasio waaminifu” Alisema Kaare
Mratibu wa Masuala ya misitu katika shirika la uhifadhi wa maliasili na Mazingira (wwf) ,Isaac Malungu amesema kuwa asilimia 90% ya nishati inayotumika nchini inatokana na kuni pamoja na mkaa hali ambayo inaathiri misitu na kutishia uhai wa maliasili nchini hivyo ameitaka serikali ihimize matumizi ya nishati mbadala ili kunusuru mazingira yanaoharibiwa kila kukicha.
Malungu alisema kuwa kilimo cha kuhama hama pamoja na ukataji miti ovyo umekua ukisababisha uharibifu wa mazingira na hata kupelekea hecta laki 4 za misitu kupotea kila mwaka kutokana na shughuli hizo.
Mkurugenzi wa Shirika la AWF,John Salehe Alisema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha hali ya ukame inayowaathiri wanyama pamoja na mimea hivyo kuathiri uhifadhi kwa ujumla .
Salehe alisema kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo upandaji wa miti pamoja na kutunza misitu ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.




Washiriki wa mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...