Hatimaye albam ya “Sura Surambi”
iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa
na mashabiki wa taarab, inazinduliwa
Alhamisi hii Novemba 26.
Albam hiyo kutoka kwao Mashauzi
Classic, itazinduliwa ndani ya ukumbi
wa Mango Garden Kinondoni huku
kundi kongwe la taarab East African
Melody, likizindikiza tukio hilo kubwa.
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha
Mashauzi ameuambia mtandao huu
kuwa albam ya “Sura Surambi”
inaundwa na nyimbo sita kali.
Ni Alhamisi ya kihistoria ambayo Isha
anaitaja kuwa itapambwa na ratiba
iliyokwenda shule itakayomwacha
mshabiki apate uhondo mwanzo
mwisho.
Isha amezitaja nyimbo hizo kuwa ni
pamoja na “Sura Surambi” aliouimba
yeye, “Kupendwa Bahati Yangu” uimbaji
wake Abdumalick Shaaban, na “Mjinga
Mpe Cheo” wa Zubeida Malick.
Nyimbo nyingine alizozitaja Isha ni
“Pendo la Ukakasi” wa Saida Ramadhan,
“Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia
Mzinga na “Mapenzi Yamenivuruga”
mwimbaji akiwa ni Naima Mohamed.
Nyimbo zote hizo sita zimetungwa na
Isha Mashauzi.
Mbali na Melody, mkali wa tungo za
mapenzi wa muziki wa kizazi kipya
Cassim Mganga naye pia atasindikiza
uzinduzi huo wa “Sura Surambi” ndani
ya Mango Garden Alhamisi hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...