Kwa takribani Wiki mbili sasa, Mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali kupanda katika Soko Kuu la Jijini Mwanza umeendelea kuwaliza watumiaji wa soko hilo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mfumuko huo unalalamikiwa na pande zote mbili kwa maana ya wauzaji na wanunuaji sokoni hapo, ambapo wameomba hatua za haraka kuchukuliwa ili kiweka mambo sawa.
Bei kwa nafaka zote sokoni hapo zimepanda bei hadi shilingi 1,000 kwa kila moja tofauti na hapo awali ambapo bidhaa iliyokuwa ikiuzwa shilingi 15,000 sasa inauzwa kati ya 2,000 hadi 2,500 ambapo steki ya nyama imepanda bei kutoka shilingi 5,000 hadi shilingi 8,000 huku nyama mchanganyiko ikiuzwa shilingi 6,000 kutoka 4,000 za awali.
Mwenyekiti wa Soko hilo Hamad Nchola amesema kuwa mfumuko huo umesababisha na mazao ya wakulima kupungua katika maghala yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa mavuno kutokana na ukosefu wa mvua katika msimu uliopita, pamoja na wafanyabiashara kutoingiza sokoni bidhaa katika kipindi cha uchaguzi mkuu, ambapo amewasihi wafanyabiashara kurejea katika mzunguko wao wa biashara kama kawaida hatua ambao itasaidia kukabiliana na mfumko huo wa bei.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu Jijini Mwanza akieleza hali ya mfumuko wa bei ilivyo sokoni hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...