MASHINDANO ya Miss Universe
Tanzania yameanza rasmi katika kumtafuta mrithi wa taji la Miss Universe Tanzania 2015 toka kwa Caroline
Bernard.
Mpaka sasa hivi waandaaji wameanza
kupokea fomu na picha za warembo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na
Zanzibar.
Miongoni mwa mikoa ambayo Miss
Universe Tanzania imepokea na inaendelea kupokea fomu na picha za washiriki ni Arusha, Mwanza, Tanga, Iringa, Mbeya na Dar es
Salaam. Zoezi la usaili na kupokea fomu kutoka mikoani litahitimishwa siku ya
Jumamos kwa kufanya usaili hapa Dar es salaam katika ukumbi wa King Solomon’s
uliopo Kinondoni mkabala na Best Bite.
Warembo wote wenye sifa wanaombwa
wajitokeze hata kama bado hawajachukua fomu kwani ukiondoa kugombania taji
kubwa la Miss Universe Tanzania pia washindi wa pili na wa tatu hupata fursa ya
kushiriki katika mashindano mengine madogo ikiwemo Miss Earth kwenda kushindana
kimataifa kama wenzao waliotangulia.
Mashindano ya Miss Universe kwa
hapa Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo Tanzania iliwakilishwa na
Flaviana Matata na kufanikiwa kuingia katika kumi bora na mwaka 2008
yaliwakilishwa na Amanda Ole Sulul, mwaka 2009 Miss Universe Tanzania
iliwakilishwa na Illuminata James,ambapo mwaka 2010 alikuwa ni Hellen Dausen,
mwaka 2011 Nelly Kamwelu, mwaka 2012 Winfrida Dominic, mwaka 2013 Betty Omara
ndiye aliyepeperusha bendera ya Tanzania na mwaka 2014 ni Caroline Bernard
ambaye ndiye anayekabidhi taji mwaka huu .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...