Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa miaka 4, na miguu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na huyo mwanaye.

Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili, hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia.
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake. Inasikitisha.
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze mchakato (process) upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.
Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-
Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
--------------------------------------
UPDATES:
Wasamaria wema kadhaa wamejitokeza kumsaidia dada Joyce. Hatuna uhakika kwamba wote wanapenda majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri upokeaji wa Tshs:
1. 505,000/-
2. 50,000/-
3.100,270/-
4. 10,000/-
5. 100,000/-
6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)
7. 500,000/- (Michuzi Media Group)
7. 800,000/- (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).
Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/- tayari zimekusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa.
Pamoja na yote hayo, kiasi cha Tshs. 3,000,000/- za ziada zinahitajika kwa ajili ya kuhitimisha zoezi lote hili. Hiyo ikiwa ni gharama za usafiri, malazi ya mgongwa na wasaidizi wawili kwa mwezi mmoja (atapopelekwa Dar es salaam kwa vipimo na matibabu) ili kumsaidia. Hivyo michango zaidi inahitajika kumuokoa dada Joyce. KUTOA NI MOYO.
Aidha, kwa kiasi kilichopatikan, mipango imeshafanywa kumpeleka dada Joyce katika hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa uchunguzi mpya wa awali. Baada ya hapo tutawafahamisha nini kinachotakiwa kuendelea.

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea sio tu kuchangia bali pia kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.

Kwa nini serikali kudai wagonjwa fedha. Ripoti hii kwa mzee Gufuli.
ReplyDeleteInasikitisha, didn't know they charge at Muhimbili.
ReplyDeleteTusiwe na jazba na kusema vitu ambavyo havitusaidii. Nani kakwambia matibabu buree??? Tatizo ni kule kutojulikana wa shida hiyo ya mgonjwa akiwa Muhimbili ambapo yaweza kuwa angesaidiwa kabla ya kufikia hali alionayo kwa sasa. Kila mwenye kujaaliwa kumsaidia basi afanye hivyo na kwa hakika Allah ametuahidi kuyakuta matendo yetu kwake
ReplyDeleteHakuna mtu au watu wanaoitwa serikali. Sisi ndio serikali, basi ni wajibu wetu tusaidiane. Leo sina mbavu lakini kama wadhungu wasemavyo. I will put my money where my mouth is.
ReplyDeleteSijui umeendelea vipi na michango kwa mama huyu.Mimi nimekuletea shs 63534 ambazo benki yasema hujenda kuchukua katika matawi ya Peoples Bank of Zanzibar moja iko Swahili/Mkungunu na nyingine iko Lumumba street.
ReplyDeleteanon
mbarikiwe wote mlioguswa na kusaidia matibabu ya mama huyu
ReplyDeletemoja kati ya matikufu ya watanzania ni hili la kusaidiana nahisi hata mingu anatukinga na mabalaa kwa moyo huu wa kusaidiana tusiache tu kidogo sana tujikamate inapobidi bila ya kujali dini kabila au rangi ya mtu
ReplyDeletekweli ni furaha mpaka chozi linatoka mungu atubariki sana
TANZANIA NA WATANZANIA KWANZA
mungu akujaalieni wote mlioguswa na kumchangia huyu mama
ReplyDelete