MBUNGE wa Nyamagana Stanslaus Mabula ameiomba Kamati
ya Maandalizi ya Tamasha la Kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, lihamie jijini Mwanza
kwa lengo la kufikisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika
Oktoba 25.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi, Alex Msama wanayafanyia kazi mapendekezo ya Mabula ili
kufanikisha tamasha hilo adhimu lenye nia ya kushukuru Mungu baada ya uchaguzi
Mkuu.Msama alisema tamasha hilo
litashirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili ambao watawasilisha
ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani
na utulivu.
Msama alisema Kamati yake
inajipanga kufikisha ujumbe wa Shukrani kwa Mungu kupitia viongozi wa dini
wakiwemo maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali hapa nchini.
“Tamasha la Kushukuru Mungu
lina mtazamo wa kufikisha asante kwa Mungu baada ya kuendelea kudumisha tunu ya
amani ambayo ndio sifa ya Tanzania nje ya mipaka,” alisema Msama.
Aidha Msama alitoa wito kwa Wadhamini
na wafadhili kujitokeza kwa lengo la kusaidia tamasha hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...