Mshindi wa shindano la muziki la Airtel Trace Music Stars Afrika
Nalimi Mayunga anatarajiwa kuondoka nchini jumatatu ya tarehe 16
novemba kwenda Marekani kwaajili ya mafunzo na kurekodi single yake
na mwanamuziki Nguli Duniani, Msenegal Akon.
Mayunga aliibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Afrika katika
mashindano yaliyoshirikisha nchi 13 barani Afrika yaliyofanyika
nchini Kenya mwanzoni mwa mwaka huu na kujishindia zawadi nono ikiwemo
deal ya kurekodi wimbo na video pamoja na kupata mafunzo ya mzuki
kutoka kwa mwana muziki Akon nchini marekani.
Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Uhusiano wa Airtel Bwana Jane
Matinde alisema" Tunajisikia furaha kuwawezesha vijana wa kitanzania
kupata fulsa na kufikia ndoto zao kupitia program zetu mbalimbali
ikiwemo hii ya Airtel Trace Music Stars. tunajivumia kumuwezesha
Mayunga na kumpatai fulsa ya kujinoa kimuziki lakini pia kutanganza
nchi yetu na muziki wetu ulimwenguni.
Ni matumaini yetu kuwa , program hii itamuwezesha mayunga na vijana
wengine watakao pata nafasi ya kushiriki kubadilisha maisha yao na
kuwa wanamuziki bora ndani na nje ya nchi na kuweza kutumia vipaji
vyao kama mtaji katika kuendesha maisha yao na famila zao kwa ujumla
Kwa upande wake Nalimi Mayunga aliwashukuru Airtel kwa kumpatia nafasi
hii ya pekee na kuhaidi kutumia fulsa hii vyema.
"kwangu huu ni muujiza wa pekee kupata nafasi ya kurekodi wimbo na
kupata mafunzo toka kwa Akon, nawashukuru sana Airtel kwani mimi
binafsi nisingeweza kuonana na Akon lakini kwa kupitia program hii na
ushindi nilioupata sasa naondoka kwenda kunolewa na kupata ujuzi toka
kwa Akon. Natoa wito kwa vijana wenzangu kutokata tamaa katika kufikia
ndoto zao na kushirikia katika mashindano kama haya pindi
yanapotangazwa kwani nao wanaweza kupata nafasi kama mimi leo
Nimejiandaa vyema kuwakilisha nchi yangu na kurekodi single yangu na
Akon hivyo naomba watanzania waendelee kuniunga mkono ili niweze kuwa
mwanamuziki nyota duniani.
Kufatia ushindi huo Airtel na Trace imesamwezesha mayunga kurekodi
single yake nchi South Afrika ijulikanayo kama " nice couple" nyimbo
hii inapatikana youtube na pia inapigwa katika vyombo mbalimbali vya
habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...