Joseph Zablon

Ufisadi na vitendo vingine vya wizi na ubadhirifu wa mali za umma nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na malezi mabaya wanayoyapata watoto toka ngazi ya familia na tatizo linakuwa kubwa zaidi anapoingia katika ajira.

Akizungumza wakati wa mahafali ya saba ya Shule za St. Andrew’s zilizopo Tabata Kisukuru, jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Wazazi (CCM), wilaya ya Ilala, Meltus Magungu alisema tabia mbaya za majumbani iiwa ni pamoja na choyo uwa na athari mbaya maofisini.

Alisema wazazi na walezi wanapaswa kukemea hali hiyo kwa nguvu zote na kuondokana na tabia inayojengeka hvi sasa ya wazazi kuwaogopa watto wao kutokana na ama viwango vyao vya elimu au vipato vinavyotokana na kazi zao. Mwenyekiti huyo alisema mtoto daima atabaki kuwa mtoto kwa wazazi wake hivyo wasiogope kuwakemea na kuwaonya pale wanapoonekana wanaenda sivyo hata kama wapo katika ajira ili kuwaepusha na vitendo hivyo ambavyo vinaligharimu Taifa mamilioni ya fedha.

Alibainisha kuwa ni jambo la kawaida kwa siku za karibuni kukuta ijana ameanza ajira lakini baada ya kipindi kifupi amekuwa na utajiri unaotia mashaka ikiwa ni pamoja na kumiliki magari ya bei mbaya ambao hayaendani na kipato chake. “Mtoto ameajirwa hata mwaka hana ana gari la bei mbaya na matumizi yasiyoeleweka, wazazi wanakaa kimya hata kumuuliza wanaogopa, kisa ana pesa? Hapo sasa nafasi yako kama mzazi inakuwa wapi?” alihoji.

Alisema kiutendo cha wazazi kushindwa kukemea mambo kama hayo kwa watoto wao ndiko ambako kumelifikisha Taifa lilipo sasa hivyo ni wajibu wa jamii kuikataa hali hiyo kwa kupigia kelele mienendo isiyofaa kwa watoto wao na pia kujenga misingi mizuri nyumbani.

Awali akizunumza wakati wa mahafai hayo, mwalimu wa zamu suleni hapo, Godwin alisema kuwa sule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya wazazi kutokulipa ada kwa wakati jambo ambalo linachelewesha maendeleo ya shule hiyo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule za St Andrew’s zilizopo Tabata Kisukuru, Martina Marcusy (kushoto), akiwaweka sawa wahitimu wa masomo ya awali katika shule hiyo kabla hawajaingia katika ukumbi wa mahafali ya saba ya shule hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Mwenyekiti wa Wazazi (CCM) wilaya ya Ilala, Meltus Magungu akimkabidhi cheti cha kuhitimu masomo ya awali kwa Mikidadi Fadhil wakati wa mahafali ya saba ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo Tabata Kisukuru, jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi wa shule hiyo, Anna Mwambije.Picha na Mpigapicha Wetu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...