Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja , wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya Ofisi za Idara ya Uhamiaji, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),akipewa maelezo alipotembelea Dawati la Mapokezi wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,Kurasini, jijijni Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...