IMG_0842
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Teresia Irafay akifungua warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili iliyojumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii iliyowaleta pamoja wadau mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na wilaya kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Loliondo
IDADI ya wanawake wanaokeketwa Loliondo wilaya ya Ngorongoro imepungua kufikia asilimia 75 kwa mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto, Loliondo, Bi. Nailejileji Joseph katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kwenye warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili.

Warsha hiyo inajumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii.

Wadau hao wanatoka ngazi mbalimbali ya vitongoji, vijiji na wilaya.
Lengo la warsha hiyo ni kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko sahihi katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Bi Nailejileji alisema idadi ya ukeketaji Loliondo inaonyesha kupungua hadi kufikia 57% mwaka 2015 ikilinganishwa na 87% mwaka 2014 kwa wanawake waliojifungulia hospitalini.
Alisema kwamba matokeo hayo yamefanikiwa kutokana na mkakati maalum unaofanyika shuleni kwa kuanzisha vituo vya kirafiki kwa vijana vinavyolenga kutoa elimu na hamasa kuhusu masuala ya ukeketaji.

Aidha mafanikio hayo ni miongoni mwa jitihada za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kueneza hamasa shirikishi katika jamii, kuelezea ukubwa wa tatizo, athari zinazotokana na ukeketaji kwa kuwashirikisha wazee wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanan) kuchukua hatua zipasazo kukomesha ukatili huu dhidi ya wasichana.
IMG_0843
Wazee wa kimila wa kimasai ni watu wenye kuheshimika na kusikilizwa kwenye jamii pale wanapotoa matamko mbalimbali yanayopelekea kuleta mabadiliko katika jamii ambao wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa katika kukomesha ukeketaji na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike ambao huozwa baada ya kufanyiwa ukeketaji mwezi Desemba kila mwaka.

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...