Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati akiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita.  
  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu walimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kila la heri ktk maisha yako mapya kama mstaafu mh. J. Kikwete.

    ReplyDelete
  2. Kila la kheri na shukran za dhati na pongezi za pekee kwako Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Nne, Mh. Jakaya Mrisho KIKWETE. Tunashkuru sana kwa kuliongoza Taifa letu la Tanzania kwa salama na amani mpaka hapo muda wako ulipofikia tamati yake na kulikabidhi kwa aliyefuata kwa salama na amani kabisa. Mola akujaaliye umri mrefu na maisha mema na kila la kheri katika maisha yako, In Sha Allah. Naamini ni kimadaraka tu, ndio imelazimu kufikia tamati, lakini bado mchango wako ungali unahitajika katika nyanja mbali mbali za maendeleo nchini na hata kwengineo utakapohitajika, naamini tungali tupo pamoja katika kulijenga na kuliendeleza Taifa letu. Mungu Ibariki Tanzania na Raia wake na Afrika kwa jumla.

    ReplyDelete
  3. It's always sad to say goodbye!

    ReplyDelete
  4. hongera na kwaheri sana mh JK kwa kweli umeliongoza taifa letu vizuri ingawaje kulikua na maadui lukuki ndani ya govt yako waliokua wakikuhujumu...tunakutakia maisha mema na marefu ... amen
    mdau wa UK

    ReplyDelete
  5. Kazi uliyoifanya imeonekana big up jk

    ReplyDelete
  6. Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  7. Big Up mkuu JK ,umefanya kazi kubwa hata wale vijana wako ffu-ughaibuni tumewasikia wakimwaga nyuzi..tukaribishane mananasi

    ReplyDelete
  8. Mheshimiwa Rais mstaafu inamaana vijana wako wa ffu-ughaibuni ndio wanalikeshesha rumba Msoga

    ReplyDelete
  9. Bongo kuiga toka lini rais mstaafu anaondoka na helicopter kuiga marekani huko Kama marine one. Afadhali ameondoka tuone huyu mpya atatatua matatizo ya afya elimu n.k kupeleka TZ kunakostahili.

    ReplyDelete
  10. Mtowa maoni wa 11 hapo juu, hii sasa ndio tabu yetu binaadamu, shida mtu asilijuwe jambo au asitoke sehemu moja akenda nyingine akatokwa na nongonongo za macho, basi tena itakuwa tabu kwa wengine na kuwaona kama washamba vile. Binafsi naona hakuna lolote la ajabu au lililoigwa hapo, ati kisa kuondoka kwa Helicopter, mie naona ni fakhari ya nchi yetu kwa kuzidi kumuenzi Raisi wetu mstaafu na kumjali kwa kila hali, sema tu binaadamu baadhi yetu siku zote huwa hatusharifiki mithli ya nguo mbovu. Ni baadhi ya silka za watu wangali wanateswa na chuki, choyo, wivu na hasama, ambavyo bado vimewaganda katika nafsi zao. Kama bongo ni waigaji, basi hata mimi na wewe tutakuwa tumeshayiiga vingi tu hapo tulipo. Binafsi nadhani kuondoka kwa style hiyo pia ni mojawapo ya maendeleo, hata angeondoka kwa 'rikwama' basi pia angenangwa, tuache kasumba za kurejeshana nyuma, badala yake tuwe ni wenye kupongeza, kutia moyo, kuhamasisha na pia kufurahia kila tunapozidi kuona mazuri na ya maendeleo katika nchi yetu. Tusiwe wenye kuponda au kukejeli.

    ReplyDelete
  11. No. 11 Umechemsha, ukiacha kula na kwenda msalani, vingine vyote mwanadamu kaiga tu. Sasa kuna shida gani our retired president kupanda chopper!!?? Tuache majungu, sisi sote dugu moja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...