Napenda
kuchukua fursa hii kuwapa pole Makamanda wenzangu wote ikiwemo Viongozi wa
Chadema Makao Makuu, Viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa, Viongozi wa Chadema
Mkoa wa Geita na wapenda Mabadiliko wote Tanzania kufuatia kifo cha Kamanda Alphonse Mawazo kilichotokea
leo tarehe 14 Novemba 2015. Kwa
kweli nimepokea taarifa ya kifo cha Kamanda Mawazo kwa mshtuko mkubwa hasa
kutokana na mazingira ya Kifo chenyewe ambayo inasemekana ameuawa kwa kuvamiwa
na kupigwa na Nondo na Mapanga na kusababisha majeraha makubwa yaliyopelekea
kutoa uhai wake. Natambua mchango mkubwa aliyotoa Alphonse Mawazo kwa kukijenga
chama katika kila kona ya Nchi yetu tangu alipohama CCM na kujiunga na Chadema.
Alphonse Mawazo ni kamanda aliyethubutu kuongea ukweli kwenye majukwaa bila
uoga. Mchango wake wa kukijenga chama hakuna wa kufananishwa naye kwa vijana wa
Chadema.
Rai yangu
Napenda
kuishauri Serikali kwa kushirikiana na Vyombo vya dola likiwemo Jeshi la Polisi
kufanya Uchunguzi wa kina kujua waliohusika na mauaji haya ya Kinyama ili
wachukuliwe hatua kali za Kisheria. Kwani muendelezo huu wa vifo tata
vinavyohusisha masuala ya Kisiasa vinajenga chuki kati ya Raia wenye itikadi tofauti
za kisiasa hosusani CCM na Vyama vya Upinzani. Pia inasababisha raia kutokuwa na imani na
Jeshi la Polisi na kuamaini kwamba linatumika katika kukandamiza demokrasia.
Vilevile muendelezo wa matukio haya unaweza kusababisha raia kukosa imani na
Serikali iliyo madarakani. Mwisho wa yote vitendo hivi visipochukuliwa hatua
stahiki vinaweza kusababisha uvunjifu mkubwa wa amani na kuondoa sifa ya
Tanzania kuwa nchi ya amani kama ilivyozoeleka.
Ni matumaini
yangu kuwa Serikali itafanya Uchunguzi wa Kina wa tukio hili kwa kuwachukulia
hatua kali wahusika ili kuondoa sintofahamu iliyojaa kwenye mawazo ya
Watanzania.
Mwenyekiti wa Chadema
Washington DC, USA
KALLEY PANDUKIZI



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...