Maafisa
masoko wa UTT-PID, Laurence Nzuki (kushoto) na Martin Mchanjila
(katikati) wakitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea kwenye banda
hilo la UTT-PID wakati wa mkutano huo wa mwaka wa Wanahisa wa UTT-AMIS
uliofanyika mwishoni mwa wiki, Novemba 21-22.2015, Ubungo Plaza jijini
Dar es Salaam.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Taasisi
ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha
(UTT-PID) inafanya miradi mbalimbali ikiwemo huduma za uuzwaji wa
viwanja katika maeneo tofauti nchini ikiwemo vile vya mradi wa katika
miji ya Chalinze na Mapinga Bagamoyo Mkoani Pwani. Pia mradi wa viwanja
vya Bunju, Tundwi songani-Kigamboni ambayo ipo Jijini Dar es Salaam.
Mingine ni Kingorwila, Madaganya, Mkoani Morogoro. Lindi, Bukoba,
Sengerema na kwingine kwingi hapa nchini.
UTT
-PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri na utendaji wa kasi
katika utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa
miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika
maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha,
uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa
majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa
majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...