Kampuni ya IVORI-IRINGA Inawataadharisha Wateja wake Hususani Wasambazaji na Wauzaji wa Maduka ya
Jumla na Reja reja kuwa, kumekuwepo na matapeli katika baadhi ya mikoa Nchini,
Wakiuza bidhaa Feki kwa kutumia jina la pipi za Ivori kwa madai ya muonekano
mpya wa bidhaa zetu.
Kampuni ya Ivori Iringa haijaubadilisha muonekano wa pipi
zake wala Nembo yake,Hakikisha kila pipi unayonunua ina nembo halisi ya Ivori kutoka Iringa.
kwa yeyote atakaenunua na Kutumia bidhaa zinazofananishwa na Pipi za Ivori Iringa na
kudhurika kiafya, basi kampuni ya ivori iringa haitahusika na malalamiko yoyote.
Ewe Mteja USIDANGANYIKE,
Nunua Pipi orijino ya Ivori Iringa
kwa usalama wa Afya yako .
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
I.F.B (LTD)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...