Na Faustine Ruta, Bukoba.

Uwanja wa Kaitaba Bukoba Umeanza kuwekwa nyasi bandia rasmi leo hii jumatatu 2 Novemba, 2015 na kutokana na maelezo ya wawekaji wamesema utachukuwa muda wa siku 14 tu. 


Wakaazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake sasa kuanza kushuhudia kipute live bila Chenga katika Uwanja huo wa Kaitaba. Timu ya Kagera Sugar nayo inatarajiwa kurudi katika Uwanja huo ambao uutumia kama Uwanja huo ambapo mpaka sasa tangu msimu uliopita wamekuwa wakitumia Viwanja vingine kwa michezo yao ya Nyumbani na Ugenini pia. 

Uwanja huu umejengwa kwa   ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects.

Uwekwaji Nyasi ukiendelea katika Uwanja wa Kaitaba leo hii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwaninin wanaweka Nyasi bandia??? Jamani tuna maji hivi hatuwezi kumwagilia kiwanja na kupanda majani yanayotakiwa na sio feki?

    ReplyDelete
  2. Faida ya nyasi bandia ni nyingi,kama vile umaridadi - muonekano wa uwanja kwa ujumla. Uniformity - hauna vipara x2 kama ambavyo nyasi halisi zilivyo na vilex2 gharama za utunzaji nyasi halisi ni kubwa ambako huusisha umwagiliaji,ukataji(fyekaji),kunyunyuzia dawa kuuwa vijidudu(herbicides ) nk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...