Na Freddy Macha
Ulikuwa na wenzio Tanzania kwa miezi sita...Mbeya vijijini. Ulikaa na wananchi. Vipi ulijisikaje katika eneo hili la Afrika?
"...Lilikuwa jambo la kipekee. Ilitupa changamoto na utofauti mkubwa, ambao sin’tokawia kulirudia tena.
Kama nilivyokueleza awali kila siku tuliyokuwa vijijini ilikuwa kama wadhifa fulani. Maana tulitaka kuwa sehemu mahsusi ya jumuiya...wenyeji walitukaribisha, walituhusisha katika mambo yao...tulikaa na familia zao, tunashukuru sana kwa hilo. Walifungua milango yao.
Wakatukaribisha.
Mara nyingi ilibidi kujifinya, na kujiuliza je kweli, Mungu wangu niko kweli Afrika?
Na hisia hiyo ya kutoamini maastajabu haikunitoka kwa miezi yote sita niliyokuwa Tanzania! Ni uzoefu ulionibadili sana. Nadhani wanavijiji wengi walikuwa na wasiwasi kwamba sisi Wazungu tulikuwa wasafi au tungeshindwa kuishi maisha yao. Ilibidi wahimizwe kuwa hakuna noma yeyote..."

Evelina na wenzake wakiwa na timu ya wanafunzi Watanzania vijijini
- Picha ya Evelina Moceviciute 2015
Wanafunzi wanavijiji Lukata na Wageni waliowafundisha taaluma ya biashara.
Picha ya Evelina Moceviciute
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...