SHIRIKA la Taifa la Hifadhi yaJamii(NSSF)
limetoa Elimu kwa Wenyeviti na Makatibu wa Wakulima wa Korosho na Ufuta wa Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi kuhusu mpango wa
Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima, Mpango huo unamwezesha mkulima kupata mikopo
mbalimbali ikiwemo mkopo wa vifaa vya kilimo pamoja na pembejeo za kilimo.
Aidha mpango huo unamwezesha mkulima na familia
yake kufaidika na mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF yakiwemo mafao ya matibabu
ambapo mkulima atapata matibabu bure yeye na familia yake.
Wanyeviti na Makatibu hao waliweza kuuliza maswali na kupata
ufafanuzi wa kina kuhusu Mpango huu kwa Wakulima na jinsi ya kuwasaidia Wakulima
kuondodokana na gharama za matibabu kupitia mafao ya matibabu yatolewayona na NSSF.
Wakulima wa Korosho wa Kilwa Masoko wakiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa Semina.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...