Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akionyesha huduma mpya ya "Airtel TV" inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
itakayowawezesha wateja wa Airtel kuangalia vipindi katika vituo
mbalimbali vya television kupitia simu zao za mkononi, akishuhudia ni
Meneja huduma za ziada wa Airtel,Prisca Tembo.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma  mpya ya "Airtel TV" itakayowawezesha wateja wa Airtel kuangalia vipindi katika vituo mbalimbali vya telesheni kupitia simu zao za mkononi.

 *   Kuunganishwa na chanel  8 za ndani na nje
  *   Kujiunga na vifurushi vya kuangalia TV bila kikomo vya siku, wiki na mwezi   Dar es Salaam, Tanzania 19 Novemba 2015, kampuni ya simu za mkononi ya  Airtel leo imezindua huduma ya ziada itakayowawezesha wateja wake nchi nzima kuangalia vipindi vya televisheni katika vituo vya ndani na nje  ya nchi kupitia simu zao za mkononi.

Huduma hii mpya ijulikanayo kama "Airtel TV" imeunganishwa na vituo 8 za televisheni vya ndani na nje ya nchi na kuwawezesha wateja wa Airtel kuangalia vipindi vilivyopita katika tamsilia wanazozipenda,
kuangalia sinema na video wanazohitaji  kupitia simu zao.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa "Airtel TV" Meneja Uhusiano wa Airtel ,
Bw Jackson Mmbando alisema "kwa kawaida mara nyingi watanzania wanaangalia vipindi vya televisheni wakiwa nyumbani  wakati wa jioni baada ya kutoka katika kazi zao. 

Tunazindua huduma yenye gharama nafuu itakayowawezesha wateja wetu kupata taarifa pindi wasipokuwapo 
majumbani mwao.

"Airtel TV" itawapatia uzoefu wa kipekee na
kuwahabarisha wateja wetu wakati wowote  wakiwa katika shughuli zao au kwenye foleni,  bila kikomo kupitia simu zao za mkononi" " huduma hiii imelenga kukidhi mahitaji ya wateja kwa kuwapatia habari  kiurahisi kwa kujiunga na kifurushi cha siku , wiki au mwezi.

Tunaamini huduma hii itapunguza uwiano wa watu wasiokuwa na fursa ya  kuangalia Televishoni na pia kuwawezesha kupata matukio kwa wakati kupitia simu zao mahali popote pale walipo" aliongeza Mmbando
Akiongea kuhusu mahudhui na jinsi ya kujiunga na huduma hiyo, Meneja
huduma za ziada ,Prisca Tembo alieleza zaidi  kuhusu dhamira yao ya
kutoa huduma yenye kiwango cha juu na gharama nafuu. 

"tunayo furaha kuwawezesha watanzania kuangalia vipindi vya televisheni kupitia simu zao kwani tunaenda sambamba na mpango wa serikali wa kidigitali wenye lengo la  kuwa na jamii kupata taarifa za yanayotokea ndani na nje ya nchi kwa wakati na kiwango cha juu.

Tembo aliongeza kwa kusema ili kupata huduma ya  "Airtel TV" mteja
anatakiwa kupakua  au kudownload application kwa kupitia linki  ya
https://goo.gl/iSvaJC kwa simu za Android na   https://goo.gl/IMvzCt
kwa simu za IOS.

Baada ya kuzi download mteja ataweza kununua kifurushi cha internet
maalum cha Televisheni  kwa kupiga *148*88#  tozo za kujiunga ni Tshs
499 kwa siku, Tshs 2,999 kwa wiki naTshs 11,999 kwa mwezi. Vituo
vinavyopatikana katika "Airtel TV" ni pamoja na Star TV, TBC, Fight
Box, 360 tune box, Citizen, FilmBox, Channel Ten na Aljazeera. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...