Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya miaka 45 ya Taifa la Oman yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Oman hapa nchini na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) tarehe 24 Novemba, 2015. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Salim Ahmed Salim. Katika hotuba yake Balozi Yahya alisifu uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Oman na kuitakia heri nchi hiyo katika kuadhimisha miaka 45. 
Balozi wa Oman hapa nchini, Mhe. Soud Al Mohammed Al-Ruqaish akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman. Pia alisifu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi yake na kuahidi kuuendeleza na kuuimarisha. 

Mhe. Mwinyi (wa kwanza kushoto) kwa pamoja na Mhe. Salim (wa pili kushoto) na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf (wa pili kulia) wakiwa kwenye sherehe hizo pamoja na wageni wengine waalikwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...