Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.

Na Mwandishi wetu,Mbeya,Jamiimojablog

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja Mkazi wa kijiji cha Malolo Ndugu Chipunguli Mkisi (30) amemuua mke wake kwa kumkata panga kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema tukio hilo la aina yake limetokea Desemba 15 mwaka huu majira ya saa 7 mchana huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia, wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya.

Msangi amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo ambaye ameuwawa na mumewe kwa kukatwa panga kichwani .

Kamanda Msangi amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

inadaiwa kuwa baada ya tukio, mtuhumiwa alijinyonga kwa kutumia kamba kwenye mti umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwake.

Aidha mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye vidole na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa na maneno “kuwa ameamua kumuua mke wake na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na mahusiana ya kimapenzi na mwanaume mwingine aitwae kilasi nzowa”

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya vwawa. ambapo kwa mujibu Kamanda Msangi uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...