Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi mpya kwenye ghorofa ya pili ya jengo la benki hiyo lililopo jengo la Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akiwa na baadhi ya wadau wa benki hiyo wakati wa kuzindua ofisi ya benki hiyo ghorofa ya pili ya benki hiyo.
Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa ofisi ya benki hiyo katika jengo la benki ya Barclays ghorofa ya pili leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akishuhudia wakati akifungua kitambaa hicho.
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...