Taswira za shughuli malumu ya chakula cha mchana iliyofanyika pale Courtyard Protea hotel ya Sea View jijini Dar es salam kwa ajili ya wazee wasiojiweza wanaosaidiwa na Asasi ya Tushikamane Pamoja Foundation siku ya Jumamosi tarehe 19 Desemba, 2015.
Shughuli iliandaliwa na uongozi wa Protea na Rickshaw kwa ajili ya kusherehekea Krismas na mwaka mpya. Jumla ya wazee 60 na wajukuu wao walikaribishwa na kusaidiwa na wafanyakazi
wa Protea. Viongozi pamoja na wahudumu waliopokea
wageni wao kwa kujituma na uchangamfu mkubwa.
Mmoja wa wazee hao akisaidiwa kuketi
Bibi akiongozwa kuketi
Pasina kujali nyadhifa zao mafisa wa Courtyard Protea hotel walisaidiana na wahudumu kuhudumia wazee hao kwa furaha na upendo
Bibi akisaidiwa kuketi mezani
Mwenyekiti wa TPF Mama Rose Mwapachu akikawashukuru Viongozi na
wafanyakazi wa Protea na Rickshaw kwa shughuli hiyo iliyofana sana
"Asante sana mwanangu..." anaonekana kusema bibi huyu wakati akiandaliwa chakula. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
impressive, Great job!
ReplyDelete