Mwimbaji wa muziki
wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini,Rebecca Malope akiwasili kwenye uwanja wa
ndege wa JNIA jioni hii tayari kwa ajili ya kutumbuiza kaika tamasha la
Krismass litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
salaam kesho likishirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa nchini
Tanzania kama vile Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa na wengine
wengi , kushoto katika picha anayefurahia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Msama Promotion iliyoandaa na kumleta mwimbaji huyo Bw. Alex Msama.
Rebecca Malope akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake (hawapo pichani) waliokuja kumlaki mara baada ya kuwasilia uwanja wa
ndege wa JNIA jioni hii tayari kwa ajili ya kutumbuiza tamasha la
Krismass litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
salaam kesho
Marope akikaribishwa kwa upendo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Msama Promotions.
Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki
wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na mratibu wa
tamasha hilo Bw. Hadson Kamoga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.
Rebecca
Malope Mwimbaji wa muziki
wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akisisitiza jambo huku
akitabasamu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati
alipowasili kwenye uwanja wa
ndege wa JNIA.
Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki
wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kuwasili nchini kwenye uwanja wa ndege wa JNIA
jijini Dar es salaam, waliosimama nyuma Bw. Alex Msama na mmoja wa
waratibu wa tamasha hilo Hadson Kamoga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...