IMG_1255 
Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ akiwa na tuzo yake ya Ijumaa Sexiest Girl 2015 baada ya kuwafunika Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

Fainali ya lile Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015 ilifanyika jana ambapo Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ aliibuka kidedea. Kidoa alitangazwa mshindi kufuatia kupigiwa kura nyingi na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa hivyo kuwafunika wenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’. 
 Akizungumza na Risasi, mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima alisema kuwa, ushindani ulikuwa mkubwa kwani wasanii wote walioshiriki walikuwa wakali ile mbaya. 
 “Kidoa amefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupigiwa kura nyingi. Atapokea tuzo, cheti pia atapewa ofa ya kutengeneza nywele kwenye saluni ya Bulldozer iliyopo Kigamboni jijini Dar kwa miezi sita pamoja na kufanyiwa shopping ya nguvu,” alisema Amran.
IMG_1250 Kidoa (katikati) akiwasalimia mashabiki baada ya kutangazwa mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2015.IMG_7945Kidoa akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Hamadombe Distributor, Fatuma Makame.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...