Na Beatrice Lyimo-Maelezo
Asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo ya uchunguzi wa makosa ya vinasaba (DNA) yanayowasilishwa katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka yanaonyesha kuwa baba si mzazi halali wa mtoto katika kesi hizo.
Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa wakala wa afya ya mazingira leo jijini Dar es Salaam.
“Kesi zinazopokelewa katika maabara yetu zinazohusu sampuli ya Vinasaba kwa mwaka zinaonyesha kuwa asilimia 49% kati ya asilimia 100% ya matokeo hayo huonyesha mzazi mmoja ambaye ni baba kuwa si mzazi halali wa mtoto huyo”.
“Vinasaba ni utambulisho wa kipekee wa kila kiumbe ambao unabeba taarifa muhimu na inayorithisha tabia au umbile fulani la mhusika. Vinasaba ni kama vile kitabu cha kumbukumbu kinachohusu maisha binafsi”, aliongeza Prof. Manyele.
Profesa Manyele aliongeza kuwa mikoa ya kanda ya Ziwa, Arusha, Dar es Salaam na Mbeya ndio inayoongoza kwa matokeo ya uchanguzi huo wa makosa ya Vinasaba nchini.
Akizungumza kuhusu lengo la mkutano huo, Profesa Manyele amesema kuwa ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya wadau wa kemikali na wadau wa afya ya mazingira kutoka katika halmashauri tofauti nchini pamoja na ofisi ya Mazingira.
Aidha Profesa alibainisha baadhi ya majukumu yanayofanywa na wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni kufanya uchunguzi ili kuhakiki ubora na usalama wa vyakula, dawa, maji, maji machafu, bidhaa za viwanda na mashambani, sampuli za mazingira na sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai.
“Matokeo ya uchunguzi wa makosa ya jinai na vinasaba (DNA) huviwezesha vyombo husika kufikia maamuzi stahili na kusaidia kutendeka kwa haki katika tuhuma za kesi za jinai ikiwemo ulevi, mauaji, ubakaji, wizi wa watoto, uhalali wa mtoto kwa mzazi, kwa kupitia vyombo husika” alifafanua Profesa.
Mbali na hayo, alisema wakala kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwasilisha mapendekezo ya kutunga sheria ya kuunda maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Sheria ya kusimamia taaluma ya Wakemia, kuimarisha upatikanaji wa mitambo na vifaa vya maabara kila teknologia inapobadilika pamoja na kuimarisha zaidi taratibu za uchunguzi ziwe za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknologia.
Matokea ya UZINZI na UGONI, wababa kubambikiwa watoto, halafu wenyewe hawana hata habari, kwa mtaji huu UKIMWI ni wetu daima milele.Ina maana 49% ni confirmed kwamba wanacheza "nje cup" kavukavu, albaki 51% kuna wengine pengine nao wanacheza nje cup sema hawakupata mimba tu, na je hao wanaume waliowazalisha 49% je nao wana wake zao, yaani mambo ni shaghalabaghala tu.
ReplyDeleteDuu, hii ina maana karibu 50% ya watanzania ni wachepukaji!!!
ReplyDeleteYAANI HII NI BALAA INA MAANA HATA HAWA NDUGU ZANGU TUMEZALIWA NA MAMA MMOJAQ HUENDA SIO BABA YETU MMOJA , HII IMEKAA VIBAYA NDIO MAANA BAADHI YA DADA ZANGU HATUFANANANI, WEE ACHA TU . VIBOGA OYEE OYEE
ReplyDeleteSasa hapa ndio mwendo mmja tu wa kuoana ndugu kwa ndugu bila kujijua. Kama mnashea DNA kwa baba mmja. Na usikute baba ana watoto kila kona kwa michepuko yake kwa wake Za wenzake
ReplyDeleteKusema kwamba asilimia 50 ya watanzania ni wachepukaji siyo kwa sababu namna ambayo hiyo statistical sample imekusanywa hairidhishi (convenience sampling) inawezekana ikawa kweli Ila ku-conclude as if it's fact, that's very immature
ReplyDeletejamani hizi taarifa ziwe zinafafanuliwa vizuri maana zinapotosha. Mimi kwangu ningetegemea iwe asilimia mia moja, kwanini? kwa sababu hawa ni wale watu wanaojikuta katika mgogoro wa kugombania watoto, na kama baba hana uhakika kwamba mtoto ni wake, basi anaamua kupima vinasaba. Kwa hiyo lazima tujue kwamba hawa ni wale tu wenye migogoro na wasio na uhakika na uhalisia wa watoto wao. Kwa maana hiyo mimi hapa ningesema kwamba asilimia 49% ya akina baba wote wanaokuwa na mashaka kwamba watoto waliozaliwa na wenza wao siyo watoto wao wamethibitisha kwa kupima vinasaba na kukuta kwamba watoto sio wa kwao, ila asilimia 51% walikuta kwamba watoto ni wa kwao. Hii ndiyo maana halisi. Maana kuna wababa wengi sana ambao hata bila kuulizwa kila mtu atajua huyo mtoto ni wake, na kuna wengine hata kama hawafanani na watoto wao, wanajua kwamba ni watoto hawana mashaka. Mpaka mtu awe na mashaka kuna kitu amekihisi. Tafadhali tuwe waangalifu katika kufanya interpretation maana tunaharibu ukweli na hili tatizo ni kubwa sana kwa waandishi wetu wa habario hapa Tanzania. Wanapotosha ukweli.!!!
ReplyDelete