
Matarajio ya kuwasili kwa ndege hizo mpya aina ya Boeing 787s ni ndani ya miezi saba ijayo, kuanzia Mei 2016, ndege hizo “Dreamliners” zenye uwezo wa kubeba abiria 299 zitaanza kutoa huduma kwenda Dusseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg kutoka Abu Dhabi zikichukua nafasi ya ndege zinazotumika sasa.
Kwa sasa Shirika la ndege la Etihad lina ndege tano tu aina ya 787s ambazo zinafanya safari zake kati ya Brisbane, Washington, Singapore na Zurich moja kwa moja kutoka Abu Dhabi.
Matarajio ya Shirika hilo ni kuongeza zaidi ya Boeing 66 ndani ya miaka kadhaa ijayo ambapo ndege hizo aina ya “Dreamliners”zitakuwa ndege rasmi za shirika hilo kwa masafa marefu.
James Hogan, ambaye ni Rais na afisa mkuu wa shirika la ndege la Etihad alisema: “Tangu kuanzishwa kwa ndege aina ya 787 ya kwanza katika huduma za kibishara mnamo februari mwaka huu, tumekuwa tukipata maoni mazuri kutoka kwa abiria wetu ambayo yamekuwa kama alama ya ubora wa hali ya juu katika kanda na dunia nzima.
“Kuanzia mwezi Mei mwakani, shirika la ndege la Etihad litazindua ndege mpya Boeing 787 aina ya dreamliners zitakazotumika rasmi badala ya hizi zilizopo kwa safari za masafa marefu ambapo zitatoa fursa kwa abiria wetu kupanda ndege za teknolojia mpya.
“Abiria na wateja wetu wa siku hizi wanapenda kusafiri bila kero wala pirika pirika kwenye usafiri wa viwango vya juu, wanataka chaguo zuri zaidi na bei nafuu. Hivi ndivyo vigezo vyao vikuu katika kuchagua na sisi hapa Etihad tunajitahidi kufikia matarajio hayo kwa tafiti na uvumbuzi wa aina mbalimbali kama vile kuleta ndege mpya na kuendelea kuboresha njia zetu za usafiri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...