MPANGO wa bima ya afya kwa njia ya simu za kiganjani unaolenga kaya maskini na sekta isiyokuwa rasmi ujulikanao kama BimaAfya umechaguliwa kushiriki katika mpango wa miezi mitatu wa kujengewa uwezo unaoitwa Startupbootcamp InsurTech utakaofanyika jijini London. 

Kupitia Startupbootcamp InsurTech, mpango wa BimaAfya utaweza kujipatia jumla ya Euro 15,000 (sh 35.3m) kwa ajili ya uwekezaji na Euro 450,000 ( zaidi ya sh 1bn) kwa ajili ya huduma mbali mbali kwenye utekelezaji wake.

Zaidi mawazo ya miradi (startups) 1,300 kutoka sehemu mbali mbali duniani yalipelekwa kuomba nafasi ya kushiriki kwenye sehemu ya kwanza ya mpango huo na10 kati ya hayo, yalijikita kwenye sekta ya afya na yalifanikiwa kuchaguliwa kushiriki.

Mpango huo wa miezi mitatu wa kujengeana uwezo unatarajia kuanza rasmi mwezi ujao jijini London Uingereza ambapo startups 10 zitapewa ofisi za kufanyia kazi kwa muda wa miezi minne bila malipo na washauri (mentors) zaidi ya 400 ambao ni wataalamu kutoka katika sekta ya fedha . Washiriki watapata nafasi ya kuyaelezea mawazo yao baada ya muda wa kujengeana uwezo kwisha.

“Utaratibu wa kuamua ni nani amefanya vizuri zaidi au mwenye wazo zuri zaidi ulikuwa ni mgumu katika historia ya mpango huu kwa sababu kila timu iliweza kuliwakilisha vyema wazo lake. Haya hivyo, 10 tu ndiyo wataweza kuchaguliwa kuwa sehemu sehemu ya mpango huu,”

BimaAfya inajenga na kusimamia mpango wa gharama nafuu kabisa wa huduma ya bima ya afya yenye manufaa makubwa. BimaAfya inawaezesha watu wa kipato cha chini na sekta isyokuwa rasmi kupata huduma zote za kiafya baada ya kuchagua huduma hiyo na kulipia kupitia simu ya kiganjani. 

BimaAfya ni utaratibu usiohusisha ujazaji wa fomu za karatasi ili kuweza kunufaika na huduma za afya kupitia bima. Mtumiaji wa huduma hii haitaji kuonana na mtoa bima (Insurer) ili aweze kuwa mwanachama na hivyo popote alipo anaweza kulipia kwa simu yake na kuwa mwanancha hivyo kunufaika 

Sita kati ya startup tisa zilizochaguliwa kwenye mpango huu kutoka Uingereza ni SAFER, CoVi Analytics, Rightindem, Domotz Data, Buzzmove na Quantifyle,. Nyingine ni massUp (Germany), FitSense (Singapore), na Myfuturenow.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...