RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Profesa Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadh Massawe.

Kuvunjwa kwa bodi hiyo kunatokana na utendaji mbovu wa Mamlaka hiyo kwa muda mrefu na kitendo cha kutokuchukua hatua katika vyanzo husika.

Akizungumza  na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kutenguliwa kwa uteuzi huo kunatokana na ziara alizofanya katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini uwepo wa mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana.

Amesema upotevu huo unatokana na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo ambao unatoa mwanya wa kupoteza mapato ya serikali na kutaka mfumo huo ubadilishe kufikia Desemba 11.

Waziri Mkuu, Majaliwa amesema kuwa kutokana na utendaji wa bandari huo mbovu, ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji wa makontena hayo na bila ya kuwepo kwa taarifa yeyote, hivyo amewasimamisha kazi wasimamizi 8 wa Bandari Kavu (ICD) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante pamoja na James Kamwomwa.

Wengine ambao hakuwemo kwenye ripoti hiyo ambao ni viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari lakini ni wahusika wakuu ambao ni Shaban Mngazija Aliyekuwa  Meneja Mapato, Rajab Mdoe Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu, Ibin Masoud Kaimu Mkurugenzi wa Fedha ,Apolonia Mosha Meneja wa Bandari Msaidizi (Fedha).

Waziri Mkuu, amesema kuwa katika ziara yake  kwa Shirika la Reli Nchini (TRL) alibaini matumizi mabaya ya fedha ya Sh.Bilioni 13 nje ya utaratibu ambao uchunguzi unakamilishwa kwa waliohusika. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti Bandari ya Dar es salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Tumbua MAJIPU BABA tumbua sana tu, twakuombea kwa MOLA.

    ReplyDelete
  2. Rais JPM, Waziri Mkuu KM, Katibu Mkuu OS songeni mbele tu nchi itanyoka. Majipu yakikauka tutapona.

    ReplyDelete
  3. Good job pm. We Tanzanians are lucky finally.
    Pm usisahau mikoani na wilayani wazembe kibao

    ReplyDelete
  4. The work pattern of Mr Magufuli is not clear. On the TRA issue the top of TRA and his official were pushed a side but not the board or the secretary general. But when it comes to Bandari the sweeping started from the ministry to bandari. There is no sign of continuity in the mode of cleaning. This give room for the Magufuli to be bias and create a room for favouring other who as well deserve to go. Up to now I can smell a pattern of removing ... well lets keep on looking.

    ReplyDelete
  5. your views seem to have some elements of truth but not absolutely true, lets be patient, he must have a strong reason of removing the general secretary to the ministry to bandari as you have called it, while leaving in office the general secretary to the ministry of finance which brings the image of biasness in your eyes .Mind you!,this regime is open and transparent, every evils will be tabled out whichever one does ,she/he will carry it on his/ her own shoulders, no stone will remain unturned (KAA CHONJO SAA MBAYA).

    ReplyDelete
  6. Working pattern is not clear? What do you mean by saying that? You're either one of those guys who created all this mess or a member of the family one of those thieves who are receiving justice from the Government right now. So if magufuli working pattern is not clear it means the people who are stealing from Tanzanian people money these the one who have a clear pattern and let them continueing what they are doing? I suspect you're out of your mind right now .

    ReplyDelete
  7. wewe anony hapo juu hujui unaloliongea au huelewi jinsi uongozi unavyofanya kazi nyamaza na utulie...hapa kazi tuu

    ReplyDelete
  8. Kazi yetu kuwaombea kwa Mola. Mashirika kibao ya kimataifa yamefurahi sana. Rais hajaenda nje lakini tayari wamemiminika Ikulu kuahidi kumwaga fedha kufadhili miradi ya maendeleo. Kumbe kuwa na uhusiano mzuri si lazima uende nje bali jinsi unavyoongoza kwa kusimamia maendeleo ya nchi. Namba imeisha someka. Sala nyingi sana kwa ajili yenu JPM, MKM na OS.

    ReplyDelete
  9. Keep Going ! Keep Going ! Keep Going! Aliselema Alija! Aliselema Alija Aliselema Alije! Selema Selema! Selema Magufuli ! Selema Majaliwa Selema Sefue! Good Job Guys, Keep it Up! Finally we will overcome! & God bless you all!

    ReplyDelete

  10. Jamani tupige Sala za kutosha, jibu kuu la kuomba litumbuliwe haraka, CCM ifanye uchaguzi wa mwenyekiti mpya.. kisha wampee magufuli... ndipo mtaona muzikiiii... hapa kasii.. tuu, maana full kujiachia.. sasa hivi naona bado anamuoneaa mwenyekiti na katibu aibu.

    ReplyDelete
  11. Na badoo!!

    ReplyDelete
  12. Hivi kwa style hii mi bado nataka kujua mawaziri wa nini???

    Mheshimiwa kwanini uweke mawaziri wa kukupa headache? Piga mzigo, makatibu wapo na ndo wataalam... wapige kazi. atakayeleta ujinga tupa nje.

    Hatuhitaji mawaziri narudia atleast for a yr

    ReplyDelete
  13. Hakuna aliyekywa anadhani yatafanyika haya yanayofanyika, Allah mtie nguvu Mr. President azidi kutumbua majipu, yakiuka tutaishi vizuri sana. Hapa kazi tu.

    ReplyDelete
  14. Nahisi kama sio maono, hii ni kazi ya Mungu Mwenyewe. "Let my people go"! Kwa hiyo atakaesimama njiani, Mmh!nampa pole in advance.

    ReplyDelete
  15. KILICHOTARAJIWA KIKIKAWIA KUJA, MOYO HUUGUA:BALI HAJA YA MTU IKIPATIKANA, NI MTI WA UZIMA. MITHALI 13:12, KILA LA HERI FANYENI KAZI NI USHUHUDA KWA ULIMWENGU. YAANI HUU NI USHUHUDA MTUPU. MBARIKIWE SANA.

    ReplyDelete
  16. Juhudi tunaiona tunataka nidhamu na uadilifu virudi kazini

    ReplyDelete
  17. Well may be I did not start so well at first by not conglatulating Mr President for showing signs of going towards the right direction. But I am enfacising that these are signs of moving towards the right direction as so far it is clear there is no any systematic approach towards the house cleaning or any clear strategy of the excercise. It should be beared in mind that the Nation has the culture of corruption so this 'here and there cleaning' won't help much. What is needed is clear, systematic and strategic approach to remove any room of spoiling the excercise and making it permanent characteristic in the government activities. And hand in hand the restoration of the right culture should start.
    I would like to assure Marlon and others that I do not have any relationship with anyone of the accused so far but when you are looking into serious matter such as the cleaning of the government and the nation, you have to be critic as well as constructive.
    The truth is if we build a robust system this excercise will last otherwise five years along the way, we will see someone else with similar stunts and washehereshaji wengi tu.
    Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  18. "Work pattern is not clear"

    How do you expect it to be clear whereas you smell like those who 'wanted change'? You fantasized otherwise because YOU KNEW this is what is exactly going to happen.

    Heheh,nowhere to hide!

    May God bless TZ

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...