NA BASHIR YAKUB .
BIASHARA hufanywa kwa mitindo ya aina nyingi kutegemea na mahitaji ya wahusika. Unaweza kufanya biashara kwa mtindo wa kampuni, unaweza kufanya biashara kwa mtindo wa mtu binafsi, lakini pia unaweza kufanya biashara kwa mtindo wa shirika ( firm)/ubia. Mitindo hii yote inatofautiana kiutendaji, kifaida na kiuwajibikaji (liability).
Kuhusu kampuni tumeeleza mara nyingi faida zake, aina zake, masuala ya hisa, mpaka namna ya kuunda kampuni, ada zinazostahili na kila kitu. Pia yapo makala yaliyoeleza biashara binafsi hasara na faida zake. Leo katika makala haya tutapata kuona biashara ya shirika (firm)/ubia . Tukumbuke kuwa haya yote ni mazao ya sheria na hivyo huwa tunayatizama kwa mtazamo wa sheria.
Sheria imeeleza kwa mapana kabisa aina zote hizi za biashara ili kuepusha migongano baina ya wahusika. Sura ya 345 ya sheria ya mikataba iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ndiyo inayozungumzia shirika/ubia kama tutakavyoona.
1.SHIRIKA/UBIA NI NINI.
Shirika/Ubia ni uhusiano uliopo baina ya watu wanaofanya biashara ya faida kwa pamoja . Kwa hiyo ili ubia uwepo ni lazima watu wawili au zaidi waungane na waamue kufanya biashara kwa pamoja. Hii ni kwa mujibu kifungu cha 190 cha sheria ya mikataba. Kuungana huku ili kufanya biashara sio kuunda kampuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...