Kampuni ya AFRICA MEDIA GROUP LTD (AMGL) inayomiliki kituo cha CHANNEL TEN na RADIO MAGIC FM imezindua huduma mpya ya kimtandao kupitia teknologia ya Application phone, itakayowezesha wananchi kwa ujumla kupata Habari kem kem kupitia simu zao za mkononi
Mtandao huo ambao utawawezesha watanzamaji wa Channel ten kupata habari tayari umezinduliwa ambapo mtaalum Mkuu wa kitendo cha mtandao Channel ten amesema kuwa kufanya hivyo kunawarahishia watazamaji kupata habari kwa muda muafaka mara wazipatapo
Huduma hiyo ambayo imezinduliwa rasmi mtumiaji yoyote wa simu aina ya android na ioS anaweza kupata taarifa hizo ambapo jinsi ya kupakua ataingia katika sehemu ya simu yake na kufungua play `store na kuandika channel ten Tanzania ataletewa maelezo ya jinsi ya kupata huduma ya kimtandao.
Pindi atakapopakua (download), na kui-Install atakuwa amepata huduma hiyo ambayo itakuwa katika kioo chake na pindi habari mpya inapoingia itamuonyesha alama moja kwa moja na yeye akifungua ataweza kusoma.
tumia link hii kupata huduma hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...