Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck
Sadick akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake leo
alipokutana nao kuelezea utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa DAWASCO kuhusu
usambazaji wa maji safi na salama ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Mhandisi
Cyprian Luhemeja akiongea na waandishi wa habari hawapo
pichani Dar es salaam leo alipokutana
nao kuelezea utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Serikali kuhusu usambazaji wa maji safi na
salama ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.Picha zote na Ally Daud-Maelezo.
NA ALLY DAUD-MAELEZO
Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar
es salaam (DAWASCO) limeongeza uzalishaji na usambazaji wa Maji safi na Salama kwa
wakazi wa jiji hilo hadi kufikia mita za ujazo 280,000 kwa siku ili kubabiliana
na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
uliolikumba jiji hilo hivi karibuni.
Hatua hiyo inatokana na utekelezaji
wa maagizo ya Serikali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck
Sadiki kuitaka DAWASCO kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa jiji hilo
ili kupambana na Ugonjwa wa Kipindupindu.
Akiongea na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam Mkuu wa mkoa huo Bw. Sadick amesema kuwa kufuatia maagizo
aliyoyatoa kwa shirika hilo ikiwemo kusambaza maji safi na salama kwa wananchi
pamoja na kutengeneza mifereji ya kupitsha maji taka ili yasiingiliane na
mikondo ya maji safi, DAWASCO wametekeleza kwa kiasi kikubwa maagizo hayo.
“Dawasco imehakikisha inazalisha maji
safi na salama kati ya mita za ujazo 270,000 na 280,000 kila siku kwa muda wote
tangu mlipuko ulipotokea na imehakikisha inasafisha na kusambaza kwa wananchi
yakiwa katika viwango vya ubora unaokubalika kwa ajili ya matumizi kwa
binadamu” amesema Bw. Sadick.
Ameongeza kuwa Dawasco imejenga
vizimba vya maji safi na salama kwenye
maeneo mbalimbali ambayo hayajakumbwa na yaliyokumbwa na athari za mlipuko wa
ugonjwa huo kwa jumla ya vizimba 48 ambavyo maeneo ya Kinondoni vizimba 5,
Magomeni vizimba 38 na Ilala vizimba 5.
Aidha, amesema kuwa DAWASCO kwa
kushirikiana na Ofisi ya Bonde Wami Ruvu imeanza kazi ya kusajili na kuwatambua
watu binafsi wenye visima virefu vilivyopo kisheria ambao wanauza maji kwa
wananchi ili kuvitambua na kudhibiti ubora wa maji na bei yake ambapo zoezi
hili litaendelea hadi Machi 2016.
“Dawasco imefanya jitihada za kuweka
dawa ya kuua wadudu aina ya chrolination kwenye maboza wakati wa
usajili kabla ya kuruhusiwa kufanya biashara ya kuuza maji kwa wananchi
na kuongeza sehemu za kuchota maji kwa kuwapelekea wananchi huduma hiyo wakitumia
magari yenye matanki yaliyokuwepo kutoka 12 mpaka kufika 49 kwa sasa” aliongeza
Bw.Sadick.Katika hatua nyingine Bw. Sadick
alitoa rai kwa wakazi wa jiji hilo kuendelea na tabia ya kufanya usafi mara kwa
mara ili kutokomezakabisa ugonjwa wa kipindupindu kwani kuanzia juzi hakuna
wagonjwa waliopokelewa katika vituo vyote.
Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa
DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kuwa wako katika hatua za mwisho
kukamilisha ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji machafu ili isiingiliane na
maji safi kwa wiki mbili zijazo.
“kufikia Februari mwakani tutaweza
kutoa maji safi na salama ya kutosha kwa wananchi wote wa Dar es salaam bila ya matatizo
yoyote” alisisitiza Mhandisi Cyprian.
Waheshimiwa na watendaji;
ReplyDeleteKwa heshima na taadhima isiwe tu usambazajiwa wa maji safi pia iwe utoaji wa maji taka katika jiji hili na miji mingine hapa Tanzania. Tuondoleeni maji taka tafadhalini. Kipindupindu kipo na kitakuwepo tu iwapo hamtatusaidia kuyaondosha na kuyaelekeza mbali na makazi ya watu maji taka haya. Tafadhalini na tafadhali Mkuu na watendaji wengine tutoleen maji taka mitaani mwetu. Kwa heshima na taadhima tunakuombeeni.
Mrs. B.S, Kibondo
tunaomba mje na suluhisho la uchafu kwanza mtunge sheria za kutubana sisi wananchi hasa wanaofanya kwa makusudi kutupa takataka watakavyo hasa wewe mkuu wa mkoa kumbuka wewe cheo chako ni kama rais wa mkoa so kua mbunifu kama rais wetu Magufuli sio unasubili mpaka maagizo yatoke serikalini wewe unabanwa na wewe wabane la sivyo utaishia njiani kwa kasi ya Magufuli #hapakazitu
ReplyDeleteTangazeni tender za kusomba taka kwa private entities.tender zizingatie uwezo wa makampuni hayo kufanyakazi hizo na siyo sura au majina..
ReplyDelete