Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuendesha droo ya pili ya promosheni ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 28 kutoka katika mikoa mbalimbali walipatikana. Akishuhudia ni balozi wa Airtel Mkwanjika na mtangazaji wa kipindi cha planet Bongo cha EATV Abdallah Hamisi Ambua (kushoto) akifuatiwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini , Mrisho Milao (wa pili kulia) na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma (kulia).
Balozi wa Airtel Mkwanjika na mtangazaji wa kipindi cha planet Bongo cha EATV Abdallah Hamisi Ambua (kulia) akiongea na moja ya washindi kupitia simu ya mkononi wakati wa kuendesha droo ya pili ya promosheni ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 28 kutoka katika mikoa mbalimbali walipatikana. Akishuhudia Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini , Bwana Mrisho Milao (kushoto) na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma (katikati).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...