Mwandishi Wetu

VINARA wa Ligi Daraja la Kwanza katika kundi (A) klabu ya Friends Rangers, imesajili wachezaji wanne ambao Emanuel Gabriel, Fred Cosmas, Mussa John 'Rooney' na Ramadhan Chombo 'Redondo' kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi hiyo unaotarajia kuanza hivi karibuni.

Ofisa Habari wa klabu hiyo Asha Kigundula, alisema kuwa katika kuhimalisha kikosi chao, wameamua waongeze wachezaji wanne ambao watasaidia kupandisha timu yao.

Kigundula alisema kuwa hata hivyo kikosi chao kitaenda kuweka kambi ya wiki moja Lushoto mkoani Tanga, kama sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili.

Alisema kuwepo kwa wachezaji hao ambao waliwahi kuvituzimikia klabu kubwa hapa nchini kutasaidia kujenga zaidi kikosi chao ambacho kimekuwa moto wa kuotea mbali.

Alisema katika msafara huo jumla ya watu 40, wataenda katika kambi hiyo maalum, kikiongozwa na Katibu Mkuu wa timu hiyo na Heyry Chibakasa (Herry Mzozo).

Rangers yenye maskani yake magomeni Kagera Dar es Salaam, ndiyo wanaoshika usukani wa Ligi Daraja la kwanza katika kundi A.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...