Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akizungumza huku Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akimsikiliza kwa makini.
Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa kampuni ya Magazeti ya Raia Mwema.
KATIBU
wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo ametembelea ofisi za
kampuni ya Raia Mwema inayotengeneza magazeti ya Raia Mwema
na Raia Tanzania, kwa lengo la kushukuru na kueleza mikakati ya chama
chake
.
Itakumbukwa miezi kadhaa iliyopita kabla ya uchaguzi mkuu
Nape, alitembelea vyumba vya habari akianzia na Raia Mwema kueleza pamoja na
mambo mengine namna walivyojipanga na uchaguzi ikiwemo kupata mgombea urais.
Akizungumza jana katika ofisi hizo alipokutana na wahariri
pamoja na viongozi mbalimbali wa kampuni hiyo alisema, wanafurahishwa na kasi
ya Rais John Magufuli, kwa sababu kinachotendeka sasa walikipanga hata kabla ya
uchaguzi.
“Tulitaka mtu wa aina hii, haya mabadiliko tuliyarataji
hivyo hatushituki kuyaona, tunachotaka kuwaambia wananchi tu ni kuwa baada ya
kumaliza serikalini mabadiliko yatahamia kwenye chama,” alisema Nape.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...