Na Mathew Mndeme
Tunamshukuru Mungu kwamba
Rais kateua mawaziri na serikali imeanza kazi rasmi. Kila waziri kwa sehemu
yake ameonesha kwamba ana hamasa na motisha ya kufanya kazi na kwa mara ya
kwanza (huenda tangu nipate akili) tumeshuhudia mawaziri wakianza kazi lisaa
limoja baada yakuapishwa huku kukiwa na habari kwamba h
Hii ni njema sana na ni dalili nzuri katika kujenga Tanzania mpya inayothamiawa kunywa hata juice walizoandaliwa kwenye ukumbi wa
kuapishwa.
Pamoja na kukiri huku,
ninaona hatari mbele iwapo mawaziri hawa, ambao wengi katika nafasi walizopewa
ni wanasiasa na sio wataalamu, watafanya maamuzi au kutoa maelekezo kwa haraka,
bila kuwa na taarifa sahihi kuhusu jambo husika.
Ninasema hivi kwa sababu
baadhi ya mambo ni ya kitaalamu na yanahitaji taaluma husika katika utekelezaji
wake hivyo maelekezo yanapotolewa kwamba yafanyike kwa siku/wiki/miezi kadhaa,
ni kinyume kabisa na uhalisia.
Uwezekano wa kufanyika makosa unatokana na
ukweli kwamba wakuu wa idara/taasisi/mamlaka wanaoelekezwa kutekeleza haya
maagizo, wengi wao wanaonekana kuna na hofu na kutetemeka na kila maagizo
wanayapokea tu na kuitikia bila kuwaonesha viongozi wao kwamba mengine hayatekelezeki
kwa muda au mtindo wanaotaka wao.
Mtaalamu yeyote yule katika nafasi yake,
lazima awe na uwezo wa kujiamini na kutetea utalaamu wake ikiwa ni pamoja na
kusema ukweli kwa kinachoagizwa mbele ya yeyote.
Sidhani kama kumweleza Rais,
Waziri Mkuu, Waziri, au Naibu waziri, kwamba jambo hili uliloagiza linahitaji
kuangaliuwa kitaalamu kabla ya kuchukua maamuzi ni kukosa nidhamu au kutokutii.
Ni bora ujibu kilicho sahihi uadhibiwe (sina hakika kama watafanya hivi) kuliko
kuitikia tu halafu ukashindwa au ukaenda kufanya maamuzi ya ajabu ya kitaalamu.
Ngoja nitoe mifano miwili:
Mambo ya kuheshimiana, kuogopa ogopa watu, kufuata taratibu na michakato ndio yaliyotufikisha hapa. Hata kama hatua za 'hapa kazi tu' zitakuwa na madhara, nadhani adhari zake zitakuwa ndogo kulinganisha na madhara ya uzembe, ubadhilifu na ufisadi uliokidhiri unaofanya pengo la masikini na tajiri tanzania liendele kuongezeka.
ReplyDeleteWatanzania tunawafahamu. Mara nyingi bila shuruti au kuogopa hawaendi. Nasubiri tu Mheshimiwa rais etembelee na TAKUKURU, maana siridhiki na utendaji. Kama wameshindwa kuambana na rushwa kutokana na sheria iliyoko, wana mbinu gani mbadala? Wameona hatua za hivi karibuni za kupambana na ufisadi jirani Kenya?
Speaking of development dictators? Yes, I support 100%.