Na Bashir
Yakub
Makubaliano ni sehemu
ya maisha yetu
ya kila siku.
Shughuli zetu za
kila siku hutegemea makubaliano.
Ukimkuta mtu anabeba
zege kwa ajili
ya ujenzi yupo
katika makubaliano. Ukimkuta mtu
anaendesha daladala, bodaboda yupo
katika makubaliano.
Ukimkuta mtu katika
ofisi yoyote ya
umma yupo katika makubaliano,walio kwenye ndoa
na uchumba nao ni
makubaliano, mfanyakazi wa
ndani yupo katika makubaliano.
Aliyechukua mkopo, aliyeuza, kununua nyumba au
kifaa kingine chochote
nao wote wapo
katika makubaliano. Haraka utaona kuwa
makubaliano hubeba sehemu
kubwa ya maisha yetu
ya kila siku.
Yatutosha kusema kuwa
makubaliano ndio maisha
yenyewe haswaa.Hata biashara yoyote
unayoshirikiana na mwenzako
nayo bila shaka ni
zao la makubaliano. Tutaona hapa makubaliano yenye
hadhi ya kuitwa
mkataba na ikiwa mkataba
wa maneno unakubalika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...