Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku moja wa baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Jeshi la Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone. Katika kikao hicho Abdulwakil aliwataka watumishi wa wizara yake wafanye kazi kwa uadilifu na weledi ili kuleta mafanikio ndani ya wizara hiyo muhimu katika maendeleo ya nchi.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara hiyo, Obeid Mbaga. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone wakiwaongoza wajumbe wa Baraza hilo kuimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya Katibu Mkuu kufungua kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) kuja kuzungumza na wajumbe wa kikao hicho (hawapo pichani) kabla ya kufungua rasmi kikao hicho. Kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...