Na Bashir Yakub.
Wote tunajua kuwa kila atendaye kosa sharti aadhibiwe. Na kuadhibiwa huko lazima kuwe kwa mujibu wa sheria. Pamoja na kuwa mtenda kosa hustahili adhabu bado watenda kosa hutofautiana hadhi. Hadhi hapa sio kuwa fulani ni mkuu wa mkoa au mkurugenzi na fulani ni mkulima wa kawaida kijijini Katanakya.
Hadhi ndio kama hizo zilizotajwa katika kichwa cha makala. Wapo watenda makosa lakini wakiwa na umri mdogo, wapo watenda makosa lakini wakiwa hawana akili timamu halikadhalika wapo watenda makosa lakini wakiwa na akili isiyo ya kawaida kwa maana ya akili ya ulevi.
Sheria inasemaje kuhusu hawa wote kuanzia utendaji wao makosa, kushitakiwa na kuwajibika kwao. Makala yataeleza ili tujue hadhi ya kimashitaka ya makundi haya.
1.JE MWENYE UGONJWA WA AKILI ANAWEZA KUSHITAKIWA ?.
Jibu ni ndiyo sheria haikatazi kumshitaki mwenye ugonjwa wa akili( chizi). Kuna tofauti kati ya kushitakiwa na kuwajibika. Kushitakiwa ni kumfungulia mashtaka na kuwajibika ni kupata adhabu baada ya kupatikana na hatia. Kwa hiyo kushitakiwa atashitakiwa isipokuwa sheria inatoa mwongozo kuhusu kuwajibika kwake.
Kifungu cha 13 ( 1 ) cha Kanuni za adhabu sura ya 16 kinasema kuwa mtu hatawajibika kwa kutenda kosa la jinai iwapo wakati wa kutenda kitendo hicho alikuwa katika hali ya ugonjwa wowote unaoathiri akili yake. Hiyo ni kanuni ya jumla iliyowekwa na kifungu hicho.
Hata hivyo kifungu hichohicho kimeweka masharti kuwa yapo mazingira ambayo mwenye ugonjwa wa akili atatakiwa kuwajibika. Kinasema kuwa mwenye ugonjwa wa akili hatawajibika kwa kutenda kosa la jinai iwapo tu wakati anatenda kosa alikuwa hajui anachokitenda, hana uwezo wa kutambua kuwa hapaswi kutenda kosa, na hana uwezo wa kuzuia kitendo hicho.
Hii maana yake ni kuwa ikiwa mgonjwa wa akili anao uwezo wa kujitambua wakati akitenda kosa basi atapatikana na jinai hata kama ameua kwa makusudi atahukumiwa kunyongwa. Maswali ya kitaalam(examination) atakayoulizwa mahakamani ndiyo yatakayotoa majibu ikiwa alikuwa anajitambua wakati wa kutenda kosa au lah. Hii ni kwasababu akademia ya tiba inaonesha kuwa machizi wengi si wakati wote huwa hawajitambui.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...