
Mmiliki na mwendeshaji wa kipindi cha Tuwalinde Watoto Wetu, Janet Mwenda.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Kipindi
cha Tuwalinde Watoto Wetu kilichokuwa kikirushwa na Clouds TV, Alhamisi
ya wiki hii kinatarajiwa kuanza tena kuonekana kupitia Clouds TV
Alhamisi ya Disemba 10, saa tatu kamili usiku.
Akizungumza na Dewjiblog,
Mmiliki na mwendeshaji wa kipindi hicho, Janet Mwenda amesema kuwa
kipindi cha Alhamisi hii kinatarajiwa kuja na kitu kipya tofauti na vile
walivyokizoea kuonekana hapo awali na hivyo kuwataka watazamaji kukaa
tayari kuona kipindi bora kuhusu watoto na changamoto wanazokutana nazo.
Amesema
lengo la kipindi hicho ni kuwakumbusha wazazi na walezi majukumu yao
kwa watoto wao na hatari wanazoweza kukutana nazo pindi wasiposimamiwa
vizuri na watu wanaoishi nao na kupitia kipindi hicho wanaweza kuona
maisha wanayokutana nayo watoto hao pindi wanapokuwa nje ya familia
zinazowalea.
“Kuna
mambo jamii inakuwa haiyaamini kama yanatokea na tunachofanya ni
kujaribu kuionesha jamii ni mambo gani yanawatokea watoto wanapokuwa
mtaani na tunachotaka ni wazazi watambue hatari hiyo na waweze kuwalea
vizuri watoto awe wa kwako au wa mwenzako,” amesema Janet.
Akizungumzia
kipindi cha Alhamisi hii, Janet amesema kipindi cha wiki hii kitakuwa
kinamuhusu kijana wa miaka 16 aliyekuja Dar es Salaam kutafuta maisha
baada ya kutoroka nyumbani kwao na kujiunga na makundi mabaya ya vijana
ambayo yalipelekea kuanza kujiingiza katika vitendo vya kimapenzi na
wanawake wanaofanya biashara ya kuuza mwili na kuwa katika hali ya
hatari ya kupata magonjwa ya zinaa.
Kujua
kilichofuata baada ya kujiingiza katika vitendo hivyo na hali aliyonayo
sasa kijana huyo usikose kutazama kipindi hicho alhamisi hii, Disemba
10 kupitia Clouds Tv!!!
USIKOSEEE!!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...