Grace R. Minja (Mama Laura)
1950 – 2000
Mama mpendwa, ni vigumu kuamini kwamba leo umetimiza miaka kumi na tano (15) tangu ulipoitwa na Mwenyezi Mungu tarehe 13/12/2000, siku ambayo sitaisahau katika maisha yangu, kwani ilikuwa ni siku ya majonzi makubwa na uchungu sana kwangu, kukukosa wewe Mama katika maisha yangu! Namshukuru sana Mungu kila iitwapo leo kwani amekuwa akinipa nguvu na kunifariji siku hadi siku.
Mama, kamwe sitasahau upendo, ucheshi, huruma, uchangamfu, mwongozo, hekima na busara zako kwangu. Namwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi ili hata ile siku ya mwisho tuje kuonana tena.
Unakumbukwa sana na mimi mwanao Laura, Mama yako, Kaka na dada zako pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote kwa ujumla.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...