Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza Mhandisi John Skauk (kulia)wakati wa ziara yake kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Hale. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Felchesmi Mramba. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea shughuli za uzalishaji umeme zinazoendelea kwenye mabwawa ya Hale, New Pangani Falls na Nyumba ya Mungu.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza wakati wa ziara yake kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu kilichopo Mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu Ndemanga na kushoto ni Mtaalamu kutoka Bodi ya Maji- Bonde la Pangani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akielezea jambo wakati wa ziara yake ya kukagua vituo vya kuzalisha umeme kwa kutumia maji. Kulia ni Meneja wa Vituo vya kuzalisha umeme vya Hale, New Pangani na Nyumba ya Mungu ambavyo kwa pamoja vinajulikana kama Pangani Hydro systems, Mhandisi John Skauk.
Bwawa la kuzalishia umeme lijulikanalo kama New Pangani Falls.
Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) limetakiwa kuandaa mpango madhubuti wa utitirishaji maji kutoka kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu ili kuwepo na maji ya kutosha kuzalisha umeme kwenye vituo vya Hale na New Pangani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika mabwawa ya kuzalishia umeme ya Hale na Pangani yaliyoko mkoani Tanga na bwawa la Nyumba ya Mungu la mkoani Kilimanjaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...